Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,
Josephat Gwajima amejitokeza leo na kujibu tuhuma
zilizotolewa dhidi yake na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa
wiki moja iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,
Askofu Gwajima amekanusha tuhuma za kuwa alimwambia Dk
Slaa kuwa wapo maaskofu ambao walihongwa na mgombea wa
Ukawa, Edward Lowassa na kuitwa mshenga wa mgombea
huyo.
Askofu huyo amesema kuwa hajawahi kumwambia Dk Slaa kuwa maaskofu wa Kikatoliki
wamehongwa na Lowassa ili wamchague hivyo aliyoyasema Dk Slaa ni kuwachafua viongozi hao
wa dini.
“Dk Slaa anasingizia kuwa maaskofu 30 wamehongwa na Lowassa, hii ni kuwaondolea maaskofu
kuaminika (credibility) ili waonekane kuwa hawafai” alisema Gwajima na kuongeza kuwa
“
Maaskofu wakatoliki hawakupewa rushwa, maaskofu wa KKKT hawakupewa rushwa, mimi
sikupewa rushwa’’
Wakati Dk Slaa anatangaza kustaafu siasa Septemba Mosi, alimwita kiongozi huyo wa Kiroho
kuwa ni mshenga wa Edward Lowassa kwa Chadema na kusema kuwa askofu huyo alimwambia
kuwa wapo maaskofu 30 wa Katoliki wamehongwa na Edward Lowassa.
Tazama hapa chini alichokisema Askofu Gwajima
0 comments:
Post a Comment