Breaking News: Gari ya Mbunge wa East Africa, Angela Kizigha Yapata Ajali Chanzo Kikiwa ni Ulevi

Gari la mbunge Mh. Angela Kiziga limepata ajari, gari hilo lilikuwa linaendeshwa na mtoto wake wa pekee akiwa na mpenzi wake.

Chanzo cha ajali ni ulevi wa kupindukia ambao wawili hao walikesha disco ,sasa wakati wanarudi mida ya saa 12.00 walipofika karibu na shule ya Moga Primary school walisinzia wakashindwa kukata kona kali ya kuelekea mbeni beach, gari lilienda moja kwa moja na kugonga ukuta wa shule, gari hilo ambalo bado lina no za usajili mpya aina ya VX landcruiser toleo la mwaka 2013/14 limeharibika vibaya sehemu ya mbele.

Mama yake alipofika aliamuru trafiki aitwe akapime ajari na gari livutwe kupelekwa nyumbani, yule mpenzi wa kijana wake alishuka taratibu na kuondoka na bodaboda. Mpaka naondoka trafiki alikuwa kafika na gari la kuivuta toka tegeta lilikuwa limefika, vijana hao hawakuumia kwa kuwa hawakuwa kwenye mwendo kasi.

Credit:  Jf
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment