Polisi Nchini Uganda Wamtafuta Zari Mpenzi wa Platnumz kwa Kosa la Kusambaza Picha za Ngono Kwenye Mitandao ya kijamii

Polisi nchini Uganda wametishia kumkamata kimwana mpya wa Diamond baada ya msichana huyo mrembo kudaiwa kusambaza picha za ngono kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook na WhatsApp kinyume cha sheria za Uganda.

Polisi nchini Uganda wamesema kuwa wanachunguza tukio hilo na ikibaini amehusika atakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Binti huyo anayejulikana kwa jina la Zarinah Ntale maarufu Zari. Awali, Zari alikuwa amekamatwa na polisi kutokana na video yake ya picha za ngono kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, lakini baadaye polisi walimuachia huru kwa dhamana, mwezi iliopita.

Baada ya kuachiwa huru kwa dhamana alisafiri hadi Afrika Kusini na aliporejea hadi leo hajaripoti polisi.

Msemaji wa Polisi mjini Kampala, Fred Enanga amethibitisha kwamba wanamtafuta Zari kwa lengo la kumkamata.

"Zari anatakiwa kuripoti polisi haraka iwezekanavyo. Tunataka kuzungumza naye kuhusu video ya ngono iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii," amesema Enanga.

Video ya Zari ni moja ya video nyingi zinazochunguzwa na polisi nchini Uganda.

Amesema kuhusiana na tukio hilo, Mnigeria Franklin Emuobor awali alidaiwa kuhusi kusambaza picha hizo naye pia anachunguzwa na polisi.

Wakati Zari akitafutwa na polisi nchini Uganda, yeye anaponda raha na mpenzi wake mpya, Diamond.

Chanzo: The Monitor.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment