Mchungaji Gwajima Apewa Siku 30 Kuondoa Kanisa Lake Tanganyika Packers

Kanisa la ufufuo na uzima linaloongozwa na mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima limeamuriwa kuondoa shughuli zake katika viwanja vya Tanganyika packers kawe wilayani kinondoni kutokana na wamiliki wa eneo hilo ambao na shirika la nyumba la taifa NHC kuanza shughuli za ujenzi.
Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu lemekuwa likiendesha shughuli zake za maombezi katika viwanja hivyo limekuwa likilahumiwa na wakazi wa maeneo hayo kuwa linasababisha usumbufu na kero kubwa za kelele.

Katika Barua iliyosainiwa na Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa shirika la nyumba la Taifa imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha shughuli zake lakini shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo,kwani shirika hilo limeshaanza kutumia Viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa KAWE ikiwa ni ujenzi wa makazi.
Meneja huyo ametoa siku 30 kwa Mchungaji Gwajima kujitayarisha na kuondoka katika viwanja hivyo wazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment