Mbowe Amshukia Mwenyekiti wa NEC Amwambia Chama Chake Hakitakubaliana na Vitendo vya Hujuma

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amemuonya vikali Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na Tume yake kwamba kamwe chama chake hakitakubaliana na vitendo vya hujuma ambavyo tayari tume hiyo imeanza dhidi ya chama chake na upinzani.
Mwenyekiti huyo akizungumza na baadhi ya Vyombo vya Habari vilivyoomba maoni yake baada ya NEC kutoa ratiba ya uandikishaji wa wapiga kura, alimtaka Jaji Lubuva asiwe adui wa demokrasia.
Amemwambia kitendo cha kucheza na demokrasia Kama anavyofanya kama vile anaamua suala la nyumbani kwake wakati nchi nzima iko kwenye tension ya kuhusu Daftari la Wapiga Kura na mfumo wa BVR, atajiandalia mazingira ya kuwa mtu wa kwanza kwenda ICC- Mahakama ya Kimataifa
Alimwambia pia kuwa suala la uandikishaji ni suala la kidemokrasia ambao wapo watu wameumia, kufanywa walemavu na hata kuuwawa Kwa ajili ya suala hilo.
Anapokuwa anafanya maamuzi Kama vile anafanya mzaha wa nyumbani kwake aelewe Watanzania wanamwangalia Kwa makini.
Kwa umri wake alionao na hadhi yake katika Jamii alistahili kutumia busara kuliko anazotumia kutokana na kukubali kutumika au kupokea maelekezo ya CCM kwa nia ya kukibeba chama hicho na serikali yake.
Kiongozi huyo wa upinzani bungeni aliendelea kusema Maamuzi anayofanya Lubuva na tume yake yanatengeneza tension kubwa Kwa jambo la kidemokrasia…na sasa anaweza kulazimisha Watanzania waanze kushughulika na Tume moja Kwa moja.
Naye Mkuu wa Idara na Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene amesema kuwa Mwenyekiti Mbowe amelazimika kutoa tahadhari Kwa NEC baada ya taasisi hiyo kuendelea kuonesha kuwa haiheshimu dhamana kubwa iliyonayo Kwa Watanzania na kwamba nchi imekuwa Kwenye tension ikisubiri maamuzi ya NEC tangu mwaka Jana.
Makene amesema kuwa Mwenyekiti Mbowe amemtaka Jaji Lubuva kuja na majibu ya hoja za wadau Kwenye kikao kilichoitishwa kati ya NEC na vyama vya siasa.
Chanzo: JF
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment