Waziri Nyalandu Afungukia Mimba ya Aunt Ezekiel

 Hatimaye Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini kwa leseni ya CCM, Lazaro Samwel Nyalandu na mkewe Faraja Kotta wamejibu tetesi kuwa mheshimiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson.Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini kwa leseni ya CCM, Lazaro Samwel Nyalandu akiwa na mkewe Faraja Kotta.

Awali tetesi hizo zilieleza kwamba Nyalandu na Aunt walikutana nchini Marekani kwenye hafla ya ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Kwa mujibu wa Nyalandu ambaye ni miongoni mwa waliotangaza nia ya kugombea urais mwaka huu, hilo ni jambo ambalo alipenda mno kulitolea ufafanuzi kwa kuwa lilipoandikwa watu wake wa karibu walimuuliza pia kutaka kufahamu kama kuna ukweli wowote.
"Unajua mpaka nikaanza kucheka," alisema Nyalandu.
"Unajua watu wana midomo, watu wanaweza wakachonga lakini michongo mingine inaweza ikawa haina dili kabisa.

"Hata anayechonga pia anajua anasababisha zogo ambalo anataka lizae matunda na wanajaribu kuliendeleza.
Waziri Nyalandu(kushoto) akiwa na Aunt Ezekiel Marekani.
"Nilifika kama mgeni rasmi kwenye tukio ukiwa mwaliko wa ubalozi na tukio lile lilichukua saa moja na huyo dada anayeitwa Aunt Ezekiel katika maisha yangu nimemuona siku moja, ndiyo hiyohiyo siku nimemuona, nilikuwa sijawahi kumuona tangu nizaliwe.

"Tumekutana naye akiwa mwalikwa pamoja na maDJ wengine wa Bongo Fleva katika tukio lenye watu wengi ambao ni Watanzania waishio Marekani.

"Nikiwa mgeni rasmi nikatoa vyeti, nikatoa hotuba wakanisindikiza nikaondoka. Kwa hiyo kwanza katika hali hiyo ya kuwa Amerika (Marekani) atakuwa aliniona kwa saa moja kwenye ule mkutano.
"Lakini pia nilikuwa sijawahi kumuona katika maisha yangu na sijawahi kumuona tena, yaani ni mtu ambaye sifahamiani naye," alisema Nyalandu pembeni akiwa na mkewe.CHANZO:.Globalpublishers
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment