Serikali imesema maafisa watendaji wa vijiji na mitaa wanapaswa kijiendeleza hadi kufikia elimu ya Astashahada kwa watendaji wa vijiji na mitaa na kwa watendaji wa kata ni stashahada ama shahada.
Pia imeagizwa kwamba wale wote ambao hawajafikia kiwango hicho watakuwa wamejiondoa wenyewe katika utumishi wa uma wa ngazi hizo.
Hayo yamesemwa bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Aggrey Mwanry wakati akijibu swali la mbunge wa Ngara Mh Deogratius Ntukamanzina aliyetaka kufahamu muda ambao serikali itawaondoa watendaji wenye uwezo mdogo na kuajiri vijana wenye elimu husika, kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya utumishi wa umma namba moja ya mwaka 2013
0 comments:
Post a Comment