Hali Tete: Profesa Anna Tibaijuka Atuma Kikosi kwa Mangula

Katika hali ya kunusuru nafasi yake ya ujumbe wa NEC na kamati kuu; profesa Anna Tibaijuka ametuma jopo kwa uongozi wa juu wa CCM ili kuhakikisha viongozi hao wanamnusuru asivuliwe nafasi zake ndani ya chama ambazo kwake ndo anaziona zimebakia na zinazoweza kusaidia katika uteuzi wake ndani CCM katika nafasi ubunge.

Harakati hizi zimetokana na jina lake kuchafuka sana baada ya kuhusika na kupata mgao wa ESCROW.

Profesa Anna amepoteza mvuto si tu ndani ya chama hata nje ya chama hasa jimboni kwake.

Pamoja na harakati za kujisafisha kupitia vyombo mbalimbali vya habari bado hali yake imezidi kuwa mbaya ambayo imeiweka mashakani nafasi yake ya CCM.

Jopo hilo limepewa tiketi ndege kwenda na fungu lao kwa kujitoa kwao kwenda kuwaonda viongozi wa juu hasa Makamu Mwenyekiti bara Philip Mangula, Katibu mkuu Kinana n.k.

Jopo hilo linaongozwa na bw. Pius Ngeze aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa Kagera, Mzee Kamaleki aliyewahi kuwa katibu mkuu CCM mkoa Kagera, Constancia Buhiyo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, wengine ni Amri Katibu wa CCM, Sebastian Rwaiterana, Zaidia Juma, Hemed Kantangayo, Nurani Amri na Mwalimu Bwahama.

Harakati hizi za Profesa naona kama ni jitihada za mfa maji maana kashachafuka nje ndani maana hata ndani ya CCM anaonekana hafai na amepoteza uungwaji mkono.

 Chanzo: JF
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment