Ewura Yaiagiza Tanesco Kupunguza Bei ya Umeme Kuanzia Marchi Mosi Mwaka Huu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeliagiza Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kupunguza bei za umeme kuanzia Machi Mosi mwaka huu.
Akitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi amesema kutokana na mabadiliko kwenye bei ya mafuta, thamani ya shilingi na mfumuko wa bei, gharama za kununua umeme zinatakiwa zishuke kwa asilimia 2.21.
Akifafanua amesema wateja wenye matumizi ya kawaida, bei ya umeme itashuka kutoka sh306 kwa uniti hadi sh298 kwa uniti sawa na punguzo la sh8 kwa uniti moja.
Amesema mwananchi anayenunua umeme wa sh10, 000 anapata uniti 32.6 hivi sasa, lakini baada ya punguzo hilo kwa fedha hiyo hiyo atapata uniti 33.5. Marekebisho hayo ni kwa bei ya kununua uniti ya umeme na si kwa tozo za mwezi za utoaji huduma.
“Wateja wenye biashara ndogo ndogo ambao wapo kwenye kundi la T2 wao bei zitashuka kwa sh5, wateja wa viwanda vya kati bei zitashuka kwa sh4, wateja wa viwanda vikubwa na migodi likiwemo Shirika la Umeme Zanzibar wao bei itashuka chini kwa sh3 kwa kila uniti moja,” amesema Ngamlagosi.


Hata hivyo, amesema wateja wanaotumia umeme chini ya uniti 75 kwa mwezi ambao hununua uniti moja kwa sh100 hawatanufaika na punguzo hilo kwa kuwa wanapata ruzuku kutoka kwa wateja wakubwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment