Breaking News: Wananchi Wenye Hasira Kali Wavamia Kituo cha Polisi na Kuchoma Moto

WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.

Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.

Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.


UPDATED

Gari tatu zilizosheheni FFU zimewasili mabomu yanapigwa mfululizo, sasa hivi wanasafisha barabara kwa kuzima moto na kutoa matairi njiani.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments: