Tume ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa Yashika Nafasi ya Juu Katika Kupokea Rushwa Nchini



Dk Edward Hoseah, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)Licha

Kama hajatawala mwendawazimu mmoja na akawafyeka vitanzi akina Chenge na wenziwe, nchi hii itabakia na rushwa milele!

Wamo pia maofisa TRA, mahakimu na majaji

Vyombo vya habari vyapongezwa�'vikaze buti'

ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kutakiwa kuzuia rushwa, maofisa wake wametajwa kuwa vinara wa kula rushwa, utafiti umebaini.

Aidha, utafiti uliofanywa na Afrobarometer umebaini kuwa Polisi, Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mahakimu na Majaji, nao ni vinara wa kupokea rushwa.


Akitoa matokeo ya utafiti huo jana jijini Dar es Salaam, mtafiti wa Afrobarometer ambaye pia ni mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Repoa, Rose Aiko, alisema utafiti umebaini kuwa takriban asilimia 70 ya wananchi wanaona rushwa imeongezeka kwenye ofisi za umma.

Alisema utafiti umebaini kuwa polisi ni vinara wa rushwa kwa asilimia 50, wakifuatiwa na maofisa wa TRA (37), Majaji na Mahakimu (36), Takukuru (29), Maofisa wa serikali za mitaa (25), watumishi wa umma (25), wabunge (22) na rais na maofisa wa Ikulu (14). Alisema pamoja na ongezeko hilo, wananchi hawaridhiki na juhudi za serikali katika kushughulikia rushwa.

"Asilimia 58 ya wananchi wanaona kuwa juhudi za serikali katika kushughulikia rushwa ni ndogo; wanaona ufanisi wa serikali katika kupambana na rushwa hauridhishi," alisema.

Alisema asilimia 34 ya wananchi hutoa rushwa ili wapate huduma au msaada mahakamani na asilimia hiyo hiyo hutoa rushwa ili kuepuka 'matatizo' na polisi.

Aidha, asilimia nyingine 20 hutoa rushwa ili wapate huduma kwenye hospitali za serikali wakati asilimia 14 wanatoa rushwa ili kupata barua au utambulisho wa serikali.

Alisema asilimia 58 ya Watanzania wanaona juhudi za serikali katika vita dhidi ya rushwa imedumaa.

"Watanzania wengi wanaamini rushwa imeongezeka katika kipindi cha mwaka uliopita (2013-2014) na wananchi wanapima juhudi za serikali katika vita hivi kuwa ni ndogo ikilinganishwa na ilivyokuwa muongo mmoja ulipita. Kwa ujumla, vita dhidi ya rushwa kwenye taasisi za umma imedorora," alisema.

Utafiti huo umeeleza kuwa pamoja na tafiti nyingi kueleza mwenendo wa rushwa nchini, tatizo hilo limeendelea kuwa changamoto kubwa ikitaja kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow kama mfano wa rushwa kubwa iliyotikisa nchi mwaka jana.

Aidha, vyombo vya habari vimepongezwa kwa namna ambavyo vimekuwa vikiibua na kuandika vitendo vya rushwa na wananchi wamevitaka viendelee kuandika zaidi.

Utafiti huo ulifanyika kuanzia Agosti 26 hadi Septemba 29 mwaka jana na kuhusisha wananchi 2,386.

Afrobarometer ni mradi wa utafiti ambao unafanya utafiti barani Afrika kwa nia ya kupaza sauti za wananchi kwenye masuala mbalimbali kama demokrasia. Kiuchumi na kijamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa Takukuru, Mary Moshi, alisema pamoja na rushwa kuendelea kushamiri, serikali imekuwa ikipambana na vitendo hivyo na kwamba wananchi wanazituhumu taasisi hizo kwa kuwa hawaoni watuhumiwa wakifikishwa mahakamani.

"Kuna njia nyingi sana ambazo serikali inatumia kupambana na rushwa ambazo nyingine wananchi hawawezi kuziona moja kwa moja...wananchi wanadhani kupeleka watuhumiwa mahakamani ndiyo serikali imefanyakazi."

Hata hivyo, asilimia 80 ya wananchi wanaotoa rushwa hawajaripoti vitendo hivyo huku wengine wakidai kuwa mazingira ya ushahidi ni magumu kutokana na vitendo hivyo kufanywa kwa siri.

Wananchi wengine wamependekeza kuwa raia wa kawaida wanaweza kusaidia vita dhidi ya rushwa hasa kwa kuacha kutoa rushwa.

Kwa upande wake, Prof. Marjorie Mbilinyi, alisema baada ya muongo mmoja wa mapambano dhidi ya rushwa, matokeo ya utafiti huo yanapaswa kuleta mabadiliko ili kuondoa manung'uniko ya wananchi.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alisema inasikitisha kwamba hata Takukuru ambayo ni taasisi inayotegemewa kupambana na rushwa, maofisa wake wanapokea rushwa.

Aliwataka utafiti mwingine ufanyike hadi kwenye sekta binafsi na vyama vya siasa kwa kuwa nako siyo salama.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Dk. Donald Mmari, alisema utafiti huo unatakiwa kuchukuliwa kama changamoto na kutaka ufanyiwe kazi.

CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment