Akizungumza na waandishi wa habari leo,Mwenyekiti wa chama hicho,Hassan Mhanjama amesema Mamlaka ya Usafiri wa Maji na Nchi Kavu (Sumatra) ina wajibu wa kuitisha mkutano na wadau kujadili kushuka kwa gharama ya nauli ili mwananchi aweze kunufaika bei ya kushuka kwa mafuta.
Mhanjama amesema kwa nauli ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa Kilomita 10 ya sh.400 inatakikwa kushuka na kufikia sh.300 na nauli ya mkoani ya Sh.40,000 inatakiwa kushuka na kufikia sh.30,000.
Amesema kuwa wamiliki wa Daladala na mabasi ya mikoani kusema bei ya vipuli na tairi zimepanda haihusiani na kushuka kwa bei ya mafuta kwani wakati mafuta yanapanda wanalamika na bei kupandisha hivyo sasa wanalazimika kushusha nauli zao.
0 comments:
Post a Comment