Marehemu Daudi Mwangosi |
Polisi wakiwa wanamshambulia Daudi Mwangosi |
Kesi hiyo inayoanza leo inaanza kusikilizwa leo Feb 12 -18 mwaka huu huenda hukumu ya kesi hiyo kutolewa siku ya tarehe 18 mara baada ya mashahidi kumaliza kutoa ushahidi wao ama kuendelea kikao kichacho iwapo mashahidi wote zaidi ya 17 waliopo katika kesi hiyo watashindwa kufika mara ya mwisho mtuhumiwa huyo kusomewa makosa yake mwaka jana.
Kushoto ni Polisi anaedaiwa kumuua Daud Mwangosi |
Katika kesi hiyo hali ya kutofahamu imekuwa ikijitokeza na kufanya watu kuwa na maswali zaidi baada ya 14 Februari Mwaka jana mtuhumiwa huyo mwenye namba G 2573 akiwa mahakamani hapo aliwatukana waandishi wa habari matusi ya nguoni kuwataka wasimpige picha huku akijidai kuwa muda si mrefu ataachiwa na kupambana na waandishi mitaani.
Siku hiyo(Februari 14,2012) Pasificus akiwa na jazba alisikika akisema.
“mtapiga picha sana mtakavyo lakini hamjui kama kesho tu nitatokahalafu tupambane mitaani huko. Nawaona sana mnaonipiga picha tutakuja kukutana tu” alisema mtuhumiwa huyo.
Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji chaNyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).
Chanzo: Fransis Godwin
0 comments:
Post a Comment