Breaking News: JWTZ Watoa Tamko Kali Baada ya Ajali ya Ndegevita Iliyotokea Mkoani Mwanza Leo..

Ndege ya Kivita moja ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiteketea kwa moto huku jitihada za kuuzima zikiendelea katika ajali iliyotokea leo Februari 27, 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza



Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita, Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto.

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu. 



Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments: