Uzinduzi wa katiba mpya umefanyika mkoani Kagera huku viongozi mbalimbali wakuudhuria katika uzinduzi huo.
Viongozi ambao walikuwepo ni viongozi kisiasa, kidini, ulinzi na usalama pamoja na mkuu wa mkoa wa Kagera John Mongela ambaye amesema kuwa hakuna kinachoweza kukamilika kwa asilimia mia moja hivyo kutokana na mtazamo na jinsi mwananchi atavyoielewa ndivyo aelekeze kura yake.
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa katika vitabu vitukufu vya dini vingeandikwa kwa kufuata matukio yote ya Yesu na mtume Mohamed, mpaka leo vingekuwa havijakamilika hivyo hata katiba hii pendekezwa ina mapungufu ambayo yanaweza kuendelea kufanyiwa marekebisho kwani hata Marekani walishafanya marekebisho mengi japo katiba ni ya miaka zaidi ya 200.
0 comments:
Post a Comment