Wananchi wa Geita, Mwanza, shinyanga, Kagera na Mara Wamtaka Lowasa Kugombea Urais 2015

a
Arusha, Tanzania. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Wilaya ya Busega, Dk Raphael Chegeni amesema kuwa ametumwa na wananchi wa mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Kagera, Shinyanga na Geita ili amshawishi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwania urais mwaka huu.

Dk Chegeni amesema kuwa utume huo alipewa baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa wito kwa wananchama wa CCM kushawishi watu wanaowaona wanafaa kugombea urais, wajitokeze kuwania nafasi hiyo ya juu nchini.

Akizungumza na gazeti la mwananchi mjini Arusha jana, Dk Chegeni amesema: "Wamenituma kuleta ujumbe huu kwa Mheshimiwa Lowassa hasa kutekeleza wito wa Rais Jakaya Kikwete alioutoa kwenye maadhimisho ya miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM Songea."

"Rais alisema wanachama wa CCM watumie fursa wailiyonayo kuwashawishi wana-CMM wenye uwezo kijitokeza kuwania urais."

Chanzo: Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment