Lady Jaydee: Gadner Ametongoza Wafanyakazi Wangu, Pia Kuwashika Makalio Wanawake Ndoa Yangu Ilijaa Mateso na Vibweka

Wiki hii, Lady Jaydee amewapa nafasi kubwa mashabiki wake ambao walikuwa wana kiu ya kutaka kujua ni nini kinachoendelea kati yake na mume wake Gadner G Habash wa Radio E-FM. Katika akaunti yake ya Instagram ametuma maswali na kuyajibu mwenyewe. Moja ya maswali ni kuhusu mustakabali wa ndoa yake na Gadner.

Yafuatayo ni maswali na majibu kama alivyopost kwenye Instagram.


1. Tunasikia umeachana na mume wako, Je ni kweli au uzushi?

JIBU: Hatujaachana, niliamua kumuacha

2. Kwanini umeachana/umemuacha mume wako?

JIBU: Nimemuacha kutokana na kuwa ndoa inatakiwa iwe na maelewano, furaha, amani na upendo.. ila kwa bahati mbaya vyote hivyo havikuwapo, sikuwa tayari kuendelea kuishi kwa maumivu huku niki pretend ili kuridhisha jamii.

3. Huoni kama umejishushia heshima kuachana na mume wako?

JIBU: Sioni hivyo, ila naona nilikuwa najishushia heshima zaidi kuishi na mume asiyekuwa na heshima, anaweza kutongoza na kushika wanawake makalio wakati niko jukwaani naimba. Pia, anawapa mademu magari yangu waendeshe na kuyagonga wakati niko safarini. Ukiachilia mbali vipigo. Kutembea na wahudumu wa restaurant yangu. Ushahidi ninao... niliwahi kumkuta anawashika mapaja na akakiri kosa. Bado kupigana na kuwatusi wateja pia. Kifupi ilikuwa ni ndoa ya mateso.

4. Baada ya kuachana unategemea kuolewa tena?

JIBU: Ni mapema kujihakikishia uolewaji mwingine, ila haimaanishi kuwa sitopenda tena. Hahitaji kuwa makini zaidi kuchagua mtu sahihi wa kumpa moyo wangu.

5. Kwanini usirudiane na mumeo?

JIBU: Siwezi kurudi nyuma tena, huwa nina msimamo thabiti. Mpaka kuamua kuondoka na uvumilivu nilionao mjue ni maji ya shingo... When I say never, I mean Never.

6. Uliwezaje kuishi na mume mlevi namna ile?

JIBU: Nilipoamua kuwa na iwe basi, Nilitoka bila kubeba kitu. Nikasafiri kwenda USA, nikakaa huko mwezi mzima ku-refresh na kujipima km kweli ntaweza ku move on. Niliporudi Tanzania sikukanya tena nyumbani, mpaka muda huu nnapo type na ku-post haya majibu.
Kwa ki fupi ni kuwa niliondoka bila kuaga, sikuona sababu ya kuaga

Asanteni jamani, nafikiri nimejibu yote.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment