Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Nchini Mheshimiwa William Lukuvi amesema Serikali itahakikisha inapambana na watu wote wanaofanya vitendo vya dhuluma, utapeli, unyang'anyi wa viwanja, majengo, mashamba na ardhi kwa wanyonge.
Waziri Lukuvi ametangaza azma hiyo wakati akijibu baadhi ya hoja za Wabunge waliochangia Taarifa ya Kamati ya Bunge, ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyowasilishwa na kupitishwa Bungeni mjini Dodoma.
Waziri Amebainisha kuwa anatambua kwamba hasa maeneo ya mijini kuna dhuluma nyingi zinafanyika ambapo Masikini, Yatima na Wajane wanadhulumiwa kwa kunyanganywa ardhi na majengo yao.
0 comments:
Post a Comment