Paul Makonda: Tukio la Vurugu kwa Warioba Limenipa Umaarufu

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, amesema tukio la kufanyiwa fujo aliyekuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, limempa umaarufu mkubwa na kumuwezesha kupata nafasi hiyo.

Alisema hayo alipohojiwa na kituo kimoja cha radio jijini Dar es Salaam, ambacho mtangazaji alitaka kujua kumekuwa na mazungumzo mengi kwenye mitandao ya kijamii ikielezea na kukosoa uteuzi wake.

Makonda, ambaye alikuwa mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka kundi la watu wenye malengo yanayofanana, alisema tukio hilo halijaathiri masuala yake ya kisiasa, badala yake limezidi kumpaisha.

“Kila tukio linaweza kuwa na mtazamo wa aina mbili negative (chanya) na positive (hasi). Mimi bahati mbaya najua kila tukio. Chochote kinachokuja mbele yangu ni sehemu ya kunisaidia mimi kusonga mbele,” alisema.

Alisema tukio la kufanyiwa fujo Jaji Warioba, lilimfanya kila mtu ndani na nje kumuulizia ili kumjua yeye (Makonda).

“Baada ya tukio lile, Tanzania hii na nje kila mtu alitaka kujua Paul Makonda ni nani, katokea wapi, anafanya nini, ni mtu wa namna gani, ana umbo gani? Lugha hiyo imesababisha mimi anione na kunitafuta na kupitia hivyo imempelekea kunifahamu na mimi nimemjua,” alisema Makonda.

Aliongeza: “Wale waliokuja kugundua ni propaganda za kitoto wanabaki tutakusaidia, wewe ni rafiki yetu, nimepata marafiki na napokea mawazo mengine.”

Novemba 3, mwaka huu, Jaji Warioba alifanyiwa fujo zilizosababisha kuvunjika kwa kongamano la kujadili mambo ya msingi ya kuangaliwa katika katiba inayopendekezwa, lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) na wazungumzaji wakuu walikuwa ni waliokuwa wajumbe wa tume hiyo.

Wakati wa fujo hizo Makonda alionekana akimshika Jaji Warioba na ilidaiwa alimpiga.

Credit: Nipashe
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment