Harakati Za Maboresho Daftari La Kudumu La Wapiga Kura Kuanza Juma Lijalo

Maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga kura nchini Tanzania yanatarajia kuanza Jumatatu ijayo Februari 16 na kumalizika Aprili 29 mwaka 2015.
Zoezi la  uandikishaji litaanza  katika mikoa ya Lindi, Ruvuma, Mtwara na Njombe na baadaye litahamia katika mikoa mingine.
Kwa mujibu wa  Mkuu wa Idara ya Elimu ya Mpiga Kura na Habari wa NEC, Ruth Masham amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa daftari la wapiga kura baada ya utoaji wa elimu kwa waratibu kukamilika
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema ratiba ya upigaji wa kura ya maoni ambayo ni Aprili 30 iko pale pale, kama ilivyotangazwa na Rais Jakaya Kikwete. Wakati uandikishaji huo ukianzia katika mikoa minne, utafungwa kwa kumalizia Dar es Salaam na Zanzibar.
Tume ya taifa ya uchaguzi   imesisitiza kuwa ni haki ya kila Mtanzania kujiandikisha. Hivyo basi ni vema wananchi waka tumia fursa hiyo ya kujiandikisha ili ifikapo Oktoba mwaka huu waweze kutumia haki  ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment