Zitto Kabwe: Wekeni Akiba ya Maneno




Katika kile kilichotafsiriwa kama dongo kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kiongozi wa chama cha ACT Zitto Zuberi Kabwe, ameweka maneno yanayoonesha kushangazwa na hatua ya CHADEMA kumpokea aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania Edward Lowassa.

Picha lilianza juzi usiku baada ya Zitto kupitia ukurasa wake wa Twitter, kupost picha ya kwanza ya Lowassa akiwa na viongozi wa juu wa CHADEMA akiipa ‘caption’ ya “mambo yanaendelea kutokea tusubiri chochote kwenye uchaguzi mkuu Oktoba”.

Ikiwa ni masaa machache tangu Mbunge huyo wa Monduli, kukabidhiwa kadi ya CHADEMA zito ameandika kupitia Facebook “wekeni akiba ya maneno” akiwaacha followers wake zaidi ya 25,000, kwenye mataa wasielewe alikusudia nini hasa.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Bazil Mbekini ameitafsiri sentensi hiyo kama ‘makavu’ kwa CHADEMA kwa kusahau kile walichokuwa wakimuita Lowassa fisadi, na leo wamemkaribisha kwenye chama hicho.

Crdt: Times
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment