Breaking News: Banza Stone Afariki Dunia Hivi Punde

Taarifa tulizozipata hivi punde si njema sana ni za staa wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ kwamba amefariki dunia akiwa nyumbani kwao Sinza Mori jijini Dar es Salaam alipokuwa akiuguzwa kwa muda sasa.

Taarifa za kifo chache ambazo zimekuwa zikizungumzwa kila kona hivi leo imekuwa si rahisi kuamini kwakuwa siku za hivi karibuni zilizuka taarifa za kuwa Banza Kafariki, Katika hili Sbm Broadcast Imefanikiwa kuzungumza kwa njia ya Simu kaka wa Marehemu Bwana Khamisi Ramadhani Masanja na kuthibitisha kwamba taarifa hizi za sasa ni za kweli Banza hatunaye.

Amesema kwa muda mdogo wake Banza amekuwa akisumbuliwa na Kifua pamoja na fangasi ya Kichwa. Kuhusu mipango ya mazishi hakuweza kuweka wazi kwakuwa wakati nazungumza naye kwa njia ya simu alikuwa kama mtu mwenye pilika pilika za msiba hivyo tumemvutia pumzi tutaweza kumtafuta tena kuweza kujua kinacho endelea.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment