Dk. Shein Asema Magufuli ni Mtu Mwema Wala Hana Tatizo



Mgombea Urais kwa upande wa Tanzania visiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dk. Ali Mohamed Shein amesema mgombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ni mtu mwema asiye na kashfa na wala hana tatizo na mtu yoyote.

Dk. Shein ameyasema hayo jana wakati akihutubia wananchama wa CCM na wakazi wa Zanzibar baada ya kutoka mjini Dodoma ambapo kulifanyika shughuli za kuwapitisha wagombea wa nafasi za urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi – CCM.
150712095349_ccm_je__dr_john_magufuli__ndiye__624x351_bbc_nocredit
Dk. John Magufuli, mgombea Urais kupitia chama cha CCM

Dk. Shein ameongezakuwa, amewahi kufanya kazi na Dk. Magufuli kwa muda zaidi ya miaka 9 tangu enzi za yeye alipokuwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, na kusema kuwa Magufuli ni mchapa kazi hivyo watanzania wategemee mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.

Pia Dk. Shein amekanusha uvumi unaoenezwa kwamba chama cha Mapinduzi sasahivi kina mpasuko na mgawanyiko na kusema hayo ni maneneno ya uzushi.
“Hapana chama chetu hakina mgawanyiko, sote tupo pamoja na tunategemea ushindi mkubwa baada ya uchaguzi”, alisema Dk. Shein.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment