Madiwani 10 wa CCM na UDP Wajiunga na CHADEMA Hivi Punde

Baadhi ya madiwani muda mfupi baada ya kukabidhiwa rasmi kadi za CHADEMA.


Aliyekuwa diwani kata ya Sakwe Masunga Ngagani (UDP) (Kushoto) akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa michezo Dutwa wakati wa kutambulishwa kwao kujiunga na Chadema. Kulia ni diwani wa kata ya Nyakabindi Benjamini Matondo.

Vyama viwili katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu CCM pamoja na UDP vimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wapatao 10 kutimkia katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa madai ya kuchoshwa na uongonzi wa vyama hivyo.

Akiwataja majina madiwani hao Katibu Mwenezi Chadema wilayani Bariadi Martine Mogani, alisema kuwa kati ya hao, watatu ni kutoka CCM na saba kutoka UDP ambao ni Benjamini Matondo (UDP) Nyakabindi, Shiwa Danhi (UDP) Sapiwi na Gulya Nyembe (UDP) Ihusi.

Wengine ni Ruta Mahagija (CCM) Dutwa, Nhandi Madede (UDP) Ikungulipu, Matalu Mongobusia (UDP) Mwaubingi, Andrea Henoka (UDP) Nkindwabiye, Juma Nengelo (CCM) Somanda pamoja na Masunga Ngagani (UDP) kutoka kata ya Sakwe.
Mtia nia nafasi ya Ubunge katika jimbo la Bariadi Magharibi Seni Silanga kupitia Chadema, akiongea na mamia ya wananchi katika kata ya Dutwa wakati wa kutambulishwa kwa madiwani 10 waliojiunga na chama hicho.

Crdt: Simiyu News
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment