Aliyenusurika Shambulio la Polisi Stakishari Asimulia Jinsi Mkasa Ulivyokuwa

Siku moja baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kuvamia kituo cha Polisi Stakishari kuua na kupora silaha, mmoja wa walionusurika katika tukio hilo askari Gaston Shadrack amesimulia hali ilivyokuwa.
Askari huyo aliyejeruhiwa bega la kulia na kifua kwenye uvamizi huo juzi usiku alisema alikuwa kwenye lindo kituoni hapo kabla ya wanaume wanane kufika na kudai wamedhulumiana.
“Ilikuwa saa 4 kuelekea saa 5 usiku. Lilikuja kundi la wanaume wanane wakiwa wamevaa makoti makubwa lakini hawajafunika nyuso. Walikuwa wakilalamika, “haiwezekani unidhulumu’ huku wakielekea ndani ya kituo.”
Aliongeza kuwa: “Utaratibu wetu ni lazima mtu akifika apite getini kwa mlinzi kwa ajili ya kupewa maelekezo ili aende ndani. Ila wao walitaka kwenda moja kwa moja,” alisimulia Shadrack ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Kutokana na utaratibu huo wa kuanzia getini, aliwaita watu hao kwa ajili ya kupata maelekezo ya kwenda ndani. Wakati huo akiwa na askari wenzake wanne hapo nje.
“…Kitendo cha kuwaita na kuwauliza mnakwenda wapi, wale jamaa waligeuka na kuvua makoti kumbe ndani walikuwa na bunduki. Wakaanza kutushambulia mimi na askari wenzangu ambao walianguka chini huku wengine wakifyatua risasi juu, nikageuka haraka na kulalia tumbo lakini wakati nageuka jambazi mmoja alinipiga risasi ikanipata kwenye bega la kulia na kifuani,” alisema Shadrack huku akionyesha majeraha hayo.
Alisema baada ya hapo majambazi hao waliingia kituoni na kuendelea kufyatua risasi lakini mmoja wao alibaki nje ya kituo.
“Nilitumia mwanya huo kunyanyua bunduki niliyokuwa nayo na kumfyatulia risasi akandondoka na mimi nikakimbia.”
Polisi kuzikwa na mama yake
Katika hatua nyingine, mmoja kati ya askari polisi wanne waliouawa katika tukio hilo, atazikwa siku moja na mama yake ambaye alifariki dunia baada ya kusikia kifo cha mwanaye, Koplo Gaudin.
Akizungumza na Mwananchi, Mkuu wa Polisi Ukonga, Mrakibu Mwandamizi, Jiliyo Simba alisema, mama wa askari huyo, alipoteza maisha baada ya kupokea habari za msiba wa mwanaye.
“Mama wa Koplo Gaudin alikuwa mgonjwa na alipopokea taarifa za kifo cha mwanaye naye alifariki dunia,” alisema.
cREDT: mWANANCHI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment