Rais Obama Kesho Anatarajia Kufunga Anga Ya Kenya kwa DakIKA 50

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuwasili Kenya siku ya Ijumaa

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuwasili Kenya siku ya Ijumaa

Kenya itafunga anga lake kwa muda wa dakika 50 kufuatia ujio wa Rais wa Marekani Barack Obama katika mji mkuu Nairobi siku ya Ijumaa, Mamlaka ya Anga ya nchi hiyo (KCAA) imesema.

Kuzuiwa kwa ndege kupaa umbali wa mita zaidi ya 20,000 kutoka chini utaendelea kuwepo jijini Nairobi katika kipindi cha ziara ya Obama kwa siku tatu.
Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta umeandaliwa vilivyo kwa ajili ya ziara ya Rais Barack Obama

Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta umeandaliwa vilivyo kwa ajili ya ziara ya Rais Barack Obama

Baadhi ya vyombo vya habari vya Marekani vimeikosoa KCAA kwa kuweka mikakati hiyo ya usafiri kwa ajili ya Obama.

Marekani ilitoa onyo la kusafiri kwenda Kenya mwezi Julai kufuatia ziara hiyo.
Wananchi wa Kenya wanajiandaa kumpokea Rais Obama

Wananchi wa Kenya wanajiandaa kumpokea Rais Obama

Wakenya wanajiandaa na bughudha muhimu baada ya polisi kutangaza kufungwa kwa barabara kubwa jijini Nairobi kuanzia Ijumaa.

Anga la Kenya pia litafungwa kwa dakika 40 siku ya Jumapili wakati Rais Obama atakapoondoka kuelekea Ethiopia.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment