Juma Nature: Nitagombea Ubunge Msimu Ujao

Mkongwe wa “game” ya Bongo flava nchini Juma Kassim Nature, amesema anajiandaa kugombea kiti cha Ubunge katika moja ya majimbo Dar es salaam msimu ujao 2020.

Akizungumza kupitia kipindi cha “the jump off” cha Times fm, Nature amedai dhamira hiyo alikuwa nayo mwaka huu ila kutokana na utitiri wa wasanii wengi kujitokeza msimu huu, akaamua aliweke jambo hilo “pending”.

“Nilikuwa na mpango huu mwaka huu, ila wenzangu wamejitokeza wengi sana kiasi ambacho nalazimika kuwaacha kwanza wao wawakilishe kule, alafu 2020 usishangae kuniona nipo kwenye harakati za kugombea Ubunge hapa Dar” alisema Kibla.

Katika line nyingine, mkali huyo alidai taarifa zinazosambaa kuwa yuko kwenye mazungumzo na meneja wa kundi la Yamoto band, Mkubwa Fella ili arejee TMK family si za kweli na wala hana mpango huo.

Crdt: Times

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment