Baba Levo: Sitaki Ubunge, Nataka Udiwani Tu

Mzuka wa siasa unazidi kuwapanda wasanii wengi wa Bongo Flava. Hata hivyo Baba Levo hautaki ubunge bali ametangaza nia ya kugombea udiwani kupitia chama cha ACT – Tanzania katika kata ya Mwanga Kaskazini mkoani Kigoma.

Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds FM, Baba Levo alisema anajipanga kuanzisha kitu kinachoitwa mgodi wa diwani. “Ndani ya mgodi wa diwani kutakuwa na timu ya mpira, timu ya kuogelea, kutakuwa na timu ya mabondia, timu ya bongo movie na timu ya wanamuziki,” alisema.

“Ndani ya mgodi kutakuwa na watu kama 200, baada ya kuwa na watu mia mbili, kwa sababu mimi ndo nitakuwa diwani na nitakuwa najua ni fungu gani limetoka kwaajili ya watu wa Mwanga Kaskazini, kwajili ya miradi mbalimbali yaani kazi zote zitakazohusu Mwanga Kaskazini, zitafanywa na timu ambayo ninayo mimi yaani Mgodi wa diwani.

Yaani deal zote zinazokuja tutazifanya sisi,” aliongeza rapper huyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment