Msanii wa muziki wa Taarab nchini na mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusuf
amesema ana mpango wa kuacha muziki na kuingia kwenye siasa.
Akizungumza kwenye kipindi cha Tam Tam za Mwambao cha East Africa Radio, Mzee Yusufu
alisema anatarajia kutoa album mbili za mwisho ili aweze kuachana na muziki na kujikita zaidi
kwenye siasa na usimamizi wa bendi yake.
“Muda ukifika nitaacha, lazima niache muziki kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya nje ya
muziki,” alisema.
“Na kama hivyo nikipita katika nafasi ya ubunge itabidi tu nichague moja, itabidi
kwenye muziki nisipatikane kwa asilimia mia moja hivyo wapenzi wa muziki wangu lazima waelewe
kuwa naacha muziki kwa sababu ya siasa na kazi zangu zingine ambazo ni nyingi na zinahitaji
uwepo wangu, hivyo lazima niache muziki ili niweze kukamilisha mambo mengine nikiwa nje ya
muziki.”
Crdt: EATV
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment