Ripoti Moja Imebaini Dola Millioni 14 za Kugharamia Vita Dhidi ya Ebola Nchini Sierra Leone Hazijulikani Zilipo.

Ripoti moja imebaini kwamba karibia dola millioni 14 za kugharamia vita dhidi ya ebola nchini Sierra Leone hazijulikani zilipo.
Mkaguzi mkuu amesema kuwa wizara ya afya na kituo cha kitaifa cha kukabiliana na ugonjwa wa ebola zilienda kinyume na sheria.
Mkaguzi huyo amesema kuwa taasisi hizo mbili zilishindwa kutoa stakhabadhi za kandarasi zilizotolewa kununua ambulansi na kujenga kituo cha matibabu ya ebola .
Ripoti hiyo imesema kulikuwa na malipo ya dharura mara mbili kwa wabunge na maafisa wa polisi na kwamba fedha zilipewa watu fulani badala ya mashirika ambayo wangewakilisha.
Serikali haitoa jibu lolote kuhusu ripoti hiyo.
BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment