Kutoka Bungeni: Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuangalia Namna ya Watanzania Walio Nje ya Nchi Kushiriki Katika Uchaguzi Mkuu

Serikali imelipeleka suala la watanzania walio nje ya nchi kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa tume ya taifa ya uchaguzi ili kuangalia utaratibu unaoweza kutumika ili watanzania hao wapate fursa ya kushiriki chaguzi mbalimbali.

waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda ndie aliyeyasema hayo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mh. Habibu Mnyaa aliyetaka kufahamu mpango wa serikali wa kuwashirikisha watanzania walio nje ya nchi katika chaguzi baada ya serikali kufanya hivyo kwa wajumbe wa bunge maalum la katiba waliokuwa nje ya nchi kupiga kura.

waziri mkuu amekiri uwepo wa matatizo mbalimbali ya kitaalam katika zoezi hilo baada ya majaribio ya siku za nyuma na hasa wakati huu ambapo zoezi la kuandikisha Daftari jipya la kudumu la wapiga kura.

Hata hivyo ameonesha wasiwasi wake endapo vyama vya upinzani vitaridhia utaratibu huo kwa kuwa tayari walishaonesha wasiwasi katika kutumika kwa utaratibu huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment