Steve Nyerere: Sijakurupuka Kugombea Ubunge

Staa wa Bongo Movies na aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye wiki iliyopita alitangaza niua yake ya kugombe ubunge mwaka huu wa uchaguzi amedai kua hajakurupuka kuutaka ubunge kupitia jimbo la Kinondoni na kuwa ataendeleza sanaa hata akiwa mbunge.

Steve alisema..’Kwanza ninataka kuwahakikishia watanzania sijakurupuka, nimekuwa mwanachama wa chama cha Mapinduzi umoja wa vijana almost miaka 25 na sasa hivi nina miaka 29 naelekea 30 lakini vilevile nimekuwa kamanda wa vijana miaka 10 tawi la bwani kinondoni, nimekuwa mwamasishaji wa chama cha mapinduzi kitaifa kwa muda wa miaka 10

Kwa hiyo nataka kusema sijakurupuka na wala sijatamkia sifa kwasababu labda nimeona mtu Fulani amegombea na mimi basi tu nigombee hapana nimeona katika wilaya yangu ya kinondoni kuna matatizo kadhaa nani anaweza kuyatetea hayo matatiizo basi mimi ndio nitakuwa mtetezi wa wilaya wa Kinondoni pamoja na matatizo ya wasanii wetu, kuhusu kazi zangu za filamu nitakuwa nafanya kama kawaida huku nikiwa natumikia kazi za Bungeni’alisema
Credit: Millardayo.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment