Tayari Prof. Lipumba,Mbatia,Zitto na Dr. Makaidi wameshawasili ukumbini. CHADEMA hawatashiriki Mdahalo wa leo kutokana na sababu zilizowasilishwa tangu Jumatatu.
SWALI: CHANGAMOTO NA VIPAUMBELE VYA TAIFA 2015 - 2025!
LIPUMBA: Sisi CUF msingi ni haki sawa kwa watu wote; kiuchumi, kijamii na kisiasa
Changamoto ni kama zifuatavyo:
1. Lishe bora kwa akina mama wajawazito/mtoto (anataja takwimu). Zinahitajika hatua za kitaifa kutatua tatizo hili.
2. Ukosefu Ajira; umepelekea athari za matukio panyaroad, kwa sababu vijana wamekata tamaa ya maisha.
3. Ukosefu wa elimu bora; Watoto wanakwenda shule lakini hawajifunzi, elimu ya kisasa inahitajika kwa karne hii ya 21.
4. Afya; Tatizo kubwa ni maradhi yasokwisha kama Malaria, TB. Matumizi bora ya rasilimali yatasaidia kumaliza tatizo.
5. Rushwa na Ufisadi uliokithiri; Ndiyo maana mafisadi wana uwezo wa kuchukua fomu.
- Sasa ni zamu ya Makaidi, M/Kiti wa NLD.
MAKAIDI:
"Sera yetu ni uzawa kwa utumishi. Watu waweze kuwatumikia wananchi wenzao. Na tutasimamia hilo.
Changamoto zilizopo ni;
1. Utu - Viongozi hawana utu hivyo hawathamini wanaowaongoza
2. Ardhi - wageni wanavamia ardhi vijijini kwa kununua kwa bei chee kutoka kwa wananchi, ugomvi wa wakulima na wafugaji.
3. Uchumi wa nchi umedorora. Kila mwaka uchumi unapungua. thamani ya pesa kupungua ni dalili tosha kuwa uchumi unashuka.
4. Afya. Life expectancy imepungua, kutoka miaka 58 hadi 54. Watu hawawez kuzalisha wakiwa na afya mbovu.
5. Elimu: Kwa kweli elimu yetu huwezi kulinganisha na wenzetu. Kwa mfano tunapwaya hata kwenye midahalo nchi za kigeni. Elimu haitusaidii na haitufanyi kujiamini.
Anakaribishwa Zitto Kabwe:
ZITTO:
Nashukuru kwa kualikwa na napenda kuwatakia mfungo mwema waislamu wote.
Changamoto tulizonazo ni hizi zifuatazo;
1. Uchumi usiozalisha ajira na usioondoa umaskini. Sekta zinazokua haziwahusu watu moja kwa moja.
2. Huduma duni za kijamii; Elimu, afya na maji. Ndizo sababu za uchumi kutokua hivyo kupeleke serikali kupokea mapato kidogo.
3. Rushwa na ufisadi; ufisadi ni ulimbikizaji wa mali. Ni tatizo kwa sababu viongozi hawana uzalendo.
4. Nyufa; Tuna tatizo la Udini na Ukabila.
Suluhisho:
Kwenye tatizo la Uchumi na huduma za kijamii, kuwepo na Miiko ya uongozi kwa viongozi. Patenganishwe siasa na biashara! Kama mtu anafanya biashara aachane na siasa.
Nyufa: Hatuna itikadi inayounganisha Watanzania. Zamani ilikuwepo. Udini na ukabila ni itikadi. Ombwe la itikadi linaleta nyufa wa kitaifa. Ndiyo maana ACT tuna azimio la Tabora kwa ajili ya kutatua taizo hilo na kuwa na itikadi ya kitaifa.
(Matangazo yamekata)..
Swali: RUSHWA NA UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA. JE, SHERIA ZILIZOPO ZINATOSHA? KAMA HAZITOSHI KIPI KIFANYIKE?
MAKAIDI:
Tatizo ni uzalendo. Watu sio wazalendo. Nchi nyingne mtu akichaguliwa anajua anafanya kwa ajili ya nchi. Watanzania sijui tumerogwa wapi.
Kuhusu sheria, sheria zipo ila watumiaji wa sheria ndio hakuna. Kwa mfano, nchi yetu haiangaalii sana mambo ya sheria. Mauaji ya albino ni kipimo tosha.
Mimi ninaamini, ikiwa nchi hii itataka maendeleo, rushwa ipigwe vita.
LIPUMBA:
Rushwa ni adui wa haki. Ili kupambana nayo inabidi kuwe na uwazi kwenye mikataba na makampuni makubwa. watu wajue ikoje na ina maslahi gani.
Taasisi iwe na uwezo wa kushitaki, sio lazima ipeleke kwa mkurugenzi wa mashtaka. Pia viongozi watangaze mali zao. Mkapa alitangaza wakati anaingia. Ni muhimu ifanyike hata wakati wa kutoka.
ZITTO:
Tume ya Warioba ilionyesha rushwa inasababishwa na kutokuwepo na mfumo wa uwajibikaji. Mtu huweza kuwa fisadi kwa ukosefu wa mfumo.
Nilipokuwa mbunge nilihakikisha tunajenga misingi hiyo kwa kushirikiana na taasisI za bunge na wabunge wenzangu.
Sisi kama viongozi, tuwe mstari wa mbele. Pia kutokana na mazingiria ya sasa, tuanzishe chombo maalum kwa ajili ya rushwa kubwa. Ripoti kila siku zinatoka lakini baada ya siku mbili zinakuwa kimya!
Lazima turejeshe miiko ya uongozi. Ni rahisi kiongozi akibanwa naye kuwabana wa chini yake.
MBATIA:
Tatizo la rushwa ni la dunia. Kwetu tatizo ni mfumo. Cha ajabu, vyombo vinavyotakiwa visimamie sheria ndio vinaongoza kwa kula rushwa. Polisi, Mahakama, TAKUKURU.
Mifumo imejaa rushwa tupu. Ripoti ya Jaji warioba imeonyesha mambo mengi. Tuanzie wapi? Vyombo vipo. Tusikubali kuingia madarakani mikono michafu lazima tulipe fadhila.
Lazima tuwajue walioingia madarakani wameingiaje ili tuwabane!
Swali: Kilimo ni tegemeo kuu la maisha kwa wananchi, na inaweza kubadili mfumo wa uchumi uliopo sasa kwenda wa viwanda; Chama kina mkakati upi wa kuinua uchumi kwenye sekta hii?
LIPUMBA;
Kulikuwa na maneno mengi kama Kilimo Uti wa Mgongo, Kilimo kwanza lakini hayakuzaa matunda ila kumkandamiza mkulima..
(Matangazo yamekata)
Suluhisho;
- Usambazaji wa pembejeo
- Elimu kwa ya kilimo bora wakulima
- Uwekezaji kwenye sekta ya kilimo na viwanda.
Serikali inawekeza pesa chini ya 6% kwenye sekta ya kilimo. Inahitaji kuweka angalau asilimia 10% ..
ZITTO:
Sekta ya kilimo imekuwa na changamoto kubwa ya ukuaji (takwimu). Tatizo kubwa ni wakulima kunyonywa (takwimu). Uzalishaji pekee ni 'Sisal' na korosho ndio unaongoza (takwimu).
Suluhisho:
- Mfumo wa kodi mahususi kwenye sekta ya kilimo kama ilivyo kwenye sekta nyingine za madini na kadhalika
- Mfumo wa pensheni kwa wakulima, ndani yake kuwe na fao la kodi. Mfano kwa msimu uliopita (takwimu).
MBATIA:
Tanzania tuna km za mraba (takwimu). Wazazi wangu walikuwa ni wakulima hadi kupata tuzo. Nilishiriki kuanzisha kilimo kwanza na serikali miaka ya 2006.
Tatizo ni utekelezaji. Tunakidharau kilimo. Haya yakiwekwa kama msingi wa taifa kwa vyama vyote vya siasa itasaidia.
MAKAIDI:
Kwa maoni yangu serikali haipo serious kwenye hili suala. Ndio maana hata mazao na vyakula vingi vinatoka nje. Mfano (anataja mikoa na hali ya kilimo ilivyo na jinsi wakulima walivyokata tamaa).
Sera potofu za serikali zinaua kilimo. Kilimo kinaendana na viwanda na masoko. Vikikosekana hivi kilimo hakina tija!
- Sasa ni kuhusu UTAWALA BORA NA UTAWALA WA SHERIA:
Swali: Je, unakubali kwamba kupuuzwa kwa ripoti za CAG ni tatizo kubwa? Na je chama chako kina msimamo gani?
ZITTO;
Ni kweli ni tatizo kubwa. Ila sasa CAG hana mamlaka ya kukamata. Pamoja na kumsifia sana Mkapa,katika uongozi wake taarifa za CAG taarifa hazikuwa zikisomwa bungeni. Lakini kuanzia 2007 angalau zilianza kusomwa.
Ni lazima bunge liwe imara sana, liunde kamati imara zitakazosimamia taarifa za CAG kwa namna inavyotakiwa. Wananchi wachague viongozi wanaoweza kuiwajibisha serikali.
MBATIA
- (Matangazo yanakata)
.. Bunge likiimarishwa, likiwa na wabunge wa upinzani hata asilimia 40%, likaiwajibisha serikali, ripoti zote zitasimamiwa vizuri.... Jambo lingine, (Matangazo yamekata)..
LIPUMBA;
Pongezi kwa JK kwa jambo la CAG. Ni chombo kinachofanya kazi kwa uweledi sana. Lakini tatizo linakuja sasa kwenye kuchukua hatua kwenye hizo ripoti.
Bajeti yetu ya mwaka huu haitekelezeki. Yenyewe inakinzana, Ina madudu mengi. Nikiingia serikalini nitaandaa bajeti stahiki, hapa hatuna bajeti. Bajeti iliyopo inapanga matumizi makubwa kuliko mapato ya serikali.
(Matangazo yanakata)
Swali: Chama chako kitachukua hatua gani kutokomeza Ujangili?
MBATIA;
Ujangili ni tatizo kubwa. Wenzetu hawafurahii uwepo wa rasilimali zote hizi. Ndio maana inatumia viongozi wasio waadilifu kuzinunua (takwimu).
Tufanye nini? UWT wanafanya nini? Wanajua huko duniani kuna njama gani dhidi yetu?
NCCR itaangalia kwanini hili tatizo linapata kasi kubwa.. Tutalizungumza kimataifa na tutahakikisha tunampenda mama Tanzania, tunapenda rasilimali tulizonazo. Watanzania tujue thaman ya rasilimali tulizonazo. Tuzitunze ili vizazi vizikute!
MAKAIDI;
Tembo wanakufa na wataendelea kufa tu. Sio tembo peke yao, vyura na nyoka pia. Hii ni dalili serikali iliyopo haina interest. (Anatoa mfano wa kontena la Hongkong). Twiga anapandishwa ndege ki ajabu ajabu. Watu hawana uzalendo. Wanagawa tu.
Wabunge waliwahi kushitakiwa kuua tembo na silaha zikakamatwa, ila mpaka leo wapo bungeni. Serikali yetu ni zembe sana.
Tufanyeje? Ukawa ikija, itabidi tu overhaul, tuanze upya.
LIPUMBA;
Suala la ujangili linaonyesha namna nchi yetu ilivyokamatwa na ufisadi. Meno ya tembo si kama dhahabu kwamba utaificha, ni lazima ukipitisha sehemu itaonekana tu.
Tunahitaji kushirikiana na mataifa kwa kuwa ni rasilimali za dunia. Sio wote wabaya, Wapo wenye nia njema za kuhifadhi rasilimali na mazingira yetu kwa vizazi na vizazi. Zipo taasisi zenye nia ya dhati.
Majangili yaliyopo kwanza yang'olewe ili tuwalinde hawa Tembo.
ZITTO;
Ili kumaliza tatizo ni lazima uangalie ni wapi linapoanzia. Sisi ni suppliers;
Kumaliza hili tatizo, basi tusimamie Uwajibikaji (anarudia mfano wa meli) - Hatua zichukuliwe kwenye matukio kama haya. Kwa kuangalia value chain utawajua tu wanaohusika!
Kuna siku nilitania wenzangu kwamba nikiwa rais; wakati nateua waziri, nampa barua mbili, ya uteuzi na kujiuzulu, ikibainika tu kafanya sivyo nampa barua ya kuachia ngazi (kicheko).
Kwa mfano, Ukitimua mawaziri watatu tu wa maliasili ; Tembo watazidi kuzaliana (kicheko).
(Matangazo yanakata kata)..
- Mdahalo unaendelea bila sauti...
SWALI: KUHUSU MAUAJI YA ALBINO
Lipumba;
Kama watu wamebainika, na wamehukumiwa kifo, basi wauawe. Sipendi kuona watu wanakufa lakini kwa hili hakuna jinsi. Na kingine, jeshi liongeze nguvu kwenye kuwatafuta wauaji. Kama waandishi wa habari wameweza kufanya uchunguzi wa kitaalamu, kwanini polisi washindwe?
ZITTO:
Tatizo ni lile lile, kukosekana kwa mfumo wa uwajibikaji. Watu wenye ulemavu hawaka salama. Napendekeza kuwepo na shule maalum kwa ajili yao na kuimarisha ulinzi. Sina maana tuwatenge, ila ni kwa ajili ya usalama wao. Wawe huru.
MBATIA;
Utambulisho wa mwanadamu upo kwenye utu wake. Je, sisi watanzania tunajua thamani yetu? Kama tumefikia hatua hii, tujiulize, Tanzania inakwenda wapi?
Itikadi yetu ya Utu ipo kwa ajili hiyo. Kuangalia thamani ya mtu na kuithamini. Uhalali wa kuishi utatufanya tujitambua na kutokufanya unyama wa aina hiyo.
MAKAIDI;
Maalbino wataendelea kufa tu. Serikali ipo kimya sana. Nailaumu kwa sababu inazembea. Kwenye ule mkutano wa maalbino na Ikulu ambapo walipigana mpaka leo haijasemwa sababu ya wao kupigana ilikuwa ni nini. Na wale wahukumiwa mpaka leo hawajatekelezewa hukumu kwanini?
Viongozi wa dini nao wazidishe jitihada kutoa mafunzo mema..........(anaendelea kushauri serikali kuhusu namna ya kushughulikia tatizo hili).

0 comments:
Post a Comment