Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi
Musa Nati alisema watu wengine wa nne wamethibitika
kuugua kipindupindu na waliolazwa katika hospitali hizo wameonekana kuwa na dalili za
ugonjwa huo.
Alisema wodi mbili zimetengwa katika hospitali hizo kwa ajili ya wagonjwa wenye dalili hizo.
Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa wanaandaa kambi maalumu kwa ajili ya wagonjwa wa
kipindupindu katika eneo la Mburahati.
Alisema wameanza kuchukua tahadhari kwa kupuliza dawa katika maeneo yaliyoripotiwa kuwa
na mlipuko wa ugonjwa huo.
“Maeneo tuliyopuliza dawa ni Manzese, Tandale na vitongoji vya Kijitonyama katika Wilaya ya
Kinondoni,” alisema Nati
Awali, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Aziz Msuya alisema mmoja wa wagonjwa
alifariki dunia wakati akipelekwa Hospitali ya Mwananyamala na mwingine alipoteza maisha
akiwa nyumbani na mwili wake kupelekwa Hospitali ya Sinza kuhifadhiwa.
Alisema katika kuchukua tahadhari ofisi yake imetoa dawa za kunywa na za kupulizia kwa kaya
70 katika maeneo ya Kijitonyama, Mtaa wa Ali Maua.
Dk Msuya aliwataka wananchi kuchukua tahadhari pale wanapoona mgonjwa anakuwa na dalili
za ugonjwa huo ili wamuwahishe katika kituo cha afya. Pia, aliwataka kuhakikisha wananawa
mikono kila wakati wanapotoka msalani au kusalimiana kwa kushikana mikono.
“Tumeshawasiliana na wenzetu wa Bohari ya Dawa (MSD) ili kuhakikisha tunakuwa na dawa za
kutosha.”
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Sophinias Ngonyani alisema wagonjwa
waliothibitika kuwa na kipindupindu ni wawili na wengine 11 bado sampuli zao ziko maabara.
Alisema wagonjwa hao wanaendelea kupatiwa huduma wakiwa katika wodi maalumu
iliyotengwa huku wakisubiri majibu.
Alipoulizwa juu ya hatua zilizochukuliwa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo, Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alitupa mpira kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said
Meck Sadik ambaye naye alisema bado hajapewa taarifa kuhusu kuwapo kwa ugonjwa huo.
Crdt: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment