RockStar4000 Watangaza Collobo ya Alikiba na Ne-Yo

Kampuni ya RockStar4000 ambayo ndo inamsimamia msanii Alikiba imetangaza habari hiyo kupitia Instagram, habari ambayo imeibua shangwe zaidi kwa mashabiki wa Ali Kiba kwenye mtandao huo.
“Exciting News: African superstar Alikiba will be collaborating with International Superstar Ne-Yo; More news to follow #kingkiba #ROC.” Wameandika RockStar4000.
Ne-Yo atakutana na Ali Kiba kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio nchini Kenya hivi karibuni. Msanii huyo anakuwa msanii wa pili wa Marekani kufanya kazi na Ali Kiba ambapo miaka kadhaa iliyopita, R-Kelly na Ali Kiba waliimba pamoja kwenye wimbo maalum wa ‘One8’ uliwashirikisha wasanii wengi wakubwa Afrika, Hands Across The World.
Siku kadhaa zilizopita kwenye tuzo za MTV/MAMA, Ne-Yo alimtaja Diamond Platinumz kuwa msanii wa Afrika anayemkubali zaidi na kuna mpango wa kufanya kazi pamoja.
Habari hii ya Ali Kiba na Ne-Yo inaongeza nguvu zaidi kwa wadau wa muziki nchini kuamini kuwa Tanzania ina vipaji vingi vikubwa vinavyoweza kufika level ya kimataifa na kufanya vizuri.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment