Breaking News: Mkimbizi Kutoka Burundi Afariki Mkoani Kigoma Kwa Ugonjwa Usiojulikana, Azikwa Tahadhari Kubwa

MTU mmoja ambaye ni raia kutoka nchi ya Burundi amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Kigoma kwa ugonjwa usiojulikana.

Mgonjwa huyo amezikwa jana jioni kwa tahadhari zote zihusuzo magonjwa hatari ya kuambukiza.

Nguo, vitanda, mashuka na vitu vyake vyote alivyokuwa akitumia wakati wa uhai wake vimechomwa moto mara tu baada ya mwili wake kuzikwa eneo la Masanga nje kidogo ya mji wa Kigoma.

(Picha zinaonesha hatua mbalimbali toka mwili wa marehemu ulipoondolewa na wataalamu waliovaa mavazi maalumu hadi mazikoni).






Akiongea na mtandao huu daktari wa wakimbizi kutoka shirika la kusafirisha wakimbizi kwenda nje ya nchi (IOM) Dkt. Beda amesema kuwa marehemu ameishi katika kambi ya wakimbizi ya Nyalugusu Wilayani Kasulu kwa muda wa miaka mitatu yeye pamoja na familia yake.


Dkt Beda amesema kuwa marehemu Buchumi Joely (39) alifika Kigoma mwezi uliopita akiwa yeye pamoja familia yake kwa ajili ya kusafirishwa na shirika la IOM kwenda marekani.

DK Beda alisema kuwa marehemu alianza kuugua tarehe 31 ya mwezi uliopita kwa kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake kama mdomoni, kwenye fizi na machoni.


"Ilipofika tarehe juzi Agosti 8 hali yake ilizidi kuwa mbaya ndipo uongozi ulipoamua kumpeleka katika hospital ya mkoa maweni kwaajili ya matibabu zaidi" alisema Dkt Beda.


Naye Kaimu mganga mkuu wa hospital ya nkoa wa kigoma Dkt Shija Ganai amethibitishia mtandao huu kuwa walimpokea mgonjwa huyo na kumlaza katika wodi namba 8 ya Grade One.

Alisema kuwa usiku wa kuamkia leo hali ya mgonjwa ilizidi kuwa mbaya na damu zilizidi kuongezeka, na walipompima maralia alikuwa na joto la kawaida la nyuzijoto 36.

Dkt. Ganai ameeleza kuwa ilipofika alfajiri ya kuamkia leo mgonjwa huyo alifariki dunia. Amesema kwamba mpaka sasa bado haijadhibitishwa kama mgonjwa huyo amekufa kwa ugonjwa wa ebola japo alikuwa na dalili zote za ugonjwa huo.

"Tumeshatuma sampo ya damu maabara kuu ya Taifa kwa ajili vipimo ili tujue ni ugonjwa gani uliomuuwa"alisema Dkt huyo.

Aliongezea kuwa hivi sasa madaktari, manesi pamoja na ndugu wote waliokuwa wanamuhudumia mgonjwa hivi sasa wapo chini ya uangalizi maalumu wa madaktari kwa muda wa siku 21.

Crdt: Michuzi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment