Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freman Mbowe, amevunja ukimya
juu ya kinachomsibu katibu mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilibrod Slaa, ambaye
amekuwa haonekani kwenye shughuli za chama hicho.
Akifungua
mkutano wa Baraza kuu la chama hicho jijini Dar es salaam jana, Mbowe
alisema kuwa Dk. Slaa ameamua kupumzika
shughuli za chama baada ya kutofautiana na wenzake juu ya ujio wa Waziri Mkuu
wa Zamani, Edward Lowassa, ambaye atapeperusha bendera ya Chadema kupitia Umoja
wa kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuwania urais katika uchaguzi mkuu Oktoba
25, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment