Watu tisa wa familia moja wameteketea kwa
moto usiku wa kuamkia leo huko Buguruni Malapa jijini Dar es
Salaam, mashuhuda wamethibitisha.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Mtaa wa Ulam
ambapo, bibi, watoto watatu wa kike na wajukuu
watano waliokuwa wanaishi nyumba namba 40
wameteketea.
Mashuhuda wa tukio hilo wameliambia Mwanannchi Digital
kuwa baba wa familia hiyo amenusurika kwa kuwa hakuwepo nyumbani, na kwamba alirejea
baada ya kupigiwa simu na majirani kuelezwa kuzuka kwa moto huo ambao chanzo chake bado
hakijafahamika.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao walishtuka usingizini kati ya saa nane na saa tisa usiku baada ya
kusikia kelele za kuomba msaada toka kwa wanafamilia hao.
“Tulipotoka nje tulikuta moto umeshamiri na kuenea karibu nyumba nzima. Hata tulipojaribu
kufanya jitihada za uokoaji tulishindwa kabisa kufanikisha jukumu hilo” walisema, kuongeza;
“Kibaya zaidi baba mwenye nyumba hakuwepo nyumbani, alikuwa kazini kwake bandarini kwani
ni mwajiriwa wa kampuni ya huduma za makontena bandarini” walisema.
Mashuhuda hao walisema, wanafamilia hao wamekutwa wamekufa kwenye chumba kimoja hali
inayoashiria kuwa wakiwa katika harakati za kujiokoa walijikusanya pamoja.
Majirani wamesema maofisa wa Polisi na Zimamoto walifika eneo la tukio asubuhi leo na kwamba
wameanza uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment