Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba leo ametangaza kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho.
Tamko
hilo la Prof. Lipumba linahitimisha siku mbili za minong’ono na tetesi
zilizogubika medani ya kisiasa nchini kuwa kiongozi huyo anaondoka
katika chama hicho hali iliyolazimu wananchama, wapenzi na mashabiki wa
kiongozi huyo kufurika makao makuu ya chama hicho Buguruni Dar es Salaam
jana ili kujua hatma ya kiongozi wao huyo.
Akizungumzia
sababu za kujiuzulu kwake, Profesa Lipumba amesema amekerwa na hatua ya
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki
kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.
Amesema
Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye
Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi
yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga
Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi
kupitia umoja huo.
Prof.
Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za
kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na
maendeleo.
0 comments:
Post a Comment