Hatimaye Chama cha ACT –
Wazalendo kimempitisha mwenyekiti wake, Anna
Mghwira (56) kuwania urais baada ya mshauri wake,
Profesa Kitila Mkumbo aliyekuwa amechukuliwa fomu
kukataa kubeba jukumu hilo.
Sambamba na Mghwira, mkutano mkuu wa chama
hicho uliokutana jana ulimpitisha Hamad Mussa Yusuf kuwa mgombea mwenza.
Chama hicho kimefikia hatua hiyo baada ya kusota kwa siku kadhaa kutafuta mgombea
na pigo kubwa lilikuwa juzi baada ya Profesa Mkumbo kukataa.
Akisoma maazimio ya Halmashauri Kuu katika mkutano mkuu jana usiku, mshauri wa
chama hicho, Profesa Mkumbo alisema wameamua kumpitisha Mghwira kwa kuwa
anazo sifa za kuwania urais.
Alisema mwenyekiti huyo anao uwezo na sifa za kuwa rais, kwa kuwa kazi za rais
ambazo ni kufikiri, kuwa mlinzi mkuu wa umoja, tunu za Taifa na kuwa mfano bora wa
ubinadamu anazimudu.
Alisema Mghwira anaweza kufikiri na amekuwa akiandika makala mbalimbali, jambo
ambalo baadhi ya wagombea hawaliwezi kwa kuwa hata hotuba wanaandikiwa.
Baada ya kumtangaza, wajumbe wa mkutano huo walishangilia kwa mbwembwe
kumpata mgombea huyo.
Kwa uteuzi huo, Mghwira atalazimika kuachia ule wa awali wa kuwania ubunge katika
Jimbo la Singida Mjini na atakuwa na kibarua ya kutafuta wadhamini nchi nzima na
kukamilisha kazi hiyo kabla ya kurejesha fomu kwa muda aliopangiwa wa saa 7.30
mchana leo.
Akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo, Mghwira alisema Taifa linahitaji kiongozi
mwenye moyo wa nyama, mwenye upendo, uadilifu na mwenye uwezo wa
kuwaunganisha watu wote bila upendeleo.
Alisema wamechelewa kumtangaza mgombea kwa kuwa walikuwa wanatafakari kauli ya
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ya “Ikulu ni mahali patakatifu”, hivyo wamempata rais
mtakatifu.
Habari
Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe alisema ilani ya uchaguzi ya chama hicho
imejikita katika mambo matano ambayo ni hifadhi ya jamii, elimu, afya, ajira na utalii.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment