Uchambuzi wa Gazeti la Wajibika: Ukawa Wakishinda, Serikali Kuwa Tatu, Wanasiasa Wanaohama Vyama Hupotea Milele

Wanasiasa wanaohama vyama hupotea milele

SIASA siyo na haijawahi kuwa mchezo mchafu, bali kuna wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo ni vichafu!
Naam. Naikumbuka hii kauli ya Mwalimu Ndimara Tegambwage, Mbunge wa kwanza wa upinzani Muleba Kaskazini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi mwaka 1995 wakati akiwa Katibu Mwenezi wa chama hicho.

Enzi hizo baada ya ujio wa Augustine Lyatonga Mrema, chama hicho ndicho kilikuwa kikuu cha upinzani na katika Bunge la Saba kilikuwa na Wabunge 28, wakiwemo 21 wa majimbo.
***********************************************************
Lowassa vs Chadema, nani ambadili mwenzie?

KIMBUNGA cha kisiasa kinatarajiwa kuanza kuonekana wiki hii baada ya Ukawa kuridhia kwamba Edward Lowassa ndiye mgombea pekee wa urais kutoka umoja huo, akipitia Chadema.

Lakini kimbunga hicho kitaongezeka kasi  wakati Lowassa atakapochukua rasmi fomu ya kugombea urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, hali ambayo italeta mafuriko makubwa.

Natabiri kwamba mafuriko hayo yanaweza kugeuka kuwa gharika pindi Lowassa atakapoanza kutambulishwa nchi nzima, kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi.
**********************************************************
Ukawa wakishinda, serikali tatu lazima

MCHAKATO wa kutafuta Katiba Mpya utaendelea endapo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) utatinga Ikulu Oktoba mwaka huu, imefahamika.
Taarifa kutoka ndani ya Ukawa zinaeleza kwamba, umoja huo utaipitisha Rasimu ya Pili ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inapendekeza muundo wa Muungano wa Serikali Tatu.
Rasimu hiyo ya Tume ya Warioba ilipendekeza muundo wa Serikali Tatu, ambapo ile ya Muungano itakuwa ya mkataba badala ya mfumo wa sasa ulivyo.

Kwa muendelezo wa habari hizi na nyinginezo tafuta gazeti lako la Wajibika kila ifikapo Jumatatu uweze kusoma habari kemukemu kwa gharama ya Tsh.800 tu, 

Ndani ya Gazeti la Wajibika utaweza kujisomea makala mbalimbali yenye kuelimisha na kuburudisha pia bila ya kusahau Hotuba ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere utazikuta humo zikiwa zinakumbusha maeneno aliyoyanena kabla ya kufa kwake na hali jinsi ilivyo sasa kwa Taifa.

Usikose gazeti lako la wajibika kwani tupo kwaajili ya kufichua maovu yoteee yaliyofichika ndani ya Jamii mpaka Serikali .....

Kwa Maoni Tuandikie ujumbe mfupi kupitia namba +255 768  068 258
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment