Nuh Mziwanda: Nakupa Hongera Wema Sepetu kwa Kufanikiwa Kutoa Amani Katika Mapenzi Yangu Mimi Na Shilole’

Siku chache zilizopita kulienea habari ya kuhusu Nuh Mziwanda kumtongoza wema, ambapo hata hivyo Nuh Mziwanda alikanusha habari hizo, Leo katika Mtandao wa Instagram Nuh Mziwanda ametoa maneno mazito ambapo moja kwa moja yalikuwa yanamuhusu wema sepetu ambae inasemekana ndie alievujisha sauti hiyo.


Katika Mtandao wa Instagram Nuh Mziwanda ameandika “Nakupa hongera kwa kufanikiwa kutoa amani katika mapenzi yangu mimi Na zuwena’maana hukua na nia njema wewe pamoja na team yako’na hata kama ingekua kweli ungemfata pembeni zuwena na kumweleza kua bwana ako anantongoza na sauti zake hizi hapa’lakini ukaona sio ishu na kuachia mitandaoni’mradi kuniaibisha mimi pamoja na na huyo unaesema unampenda sana na ni shoga yako’.

kingine Wema umetongozwa na wangapi hapa duniani kwann usiweke Voic note zao?yani moja kwa moja umetaka kusambalatisha mapenzi yetu na now naona mnaanza kutumana kumtongoza shishi’well madam nakupa salute zako’najua unaishi kwa amani na raha ‘ila huku umekiwasha mpka mtu unakua hauna amani ya moyo na ukizingatia sijawahi hata kukaa na ww tukapga stor wala kuona undani wa mwili wangu’kipindi una kampeni uling’ang’ania sana niingie kwenye group yako ya whatsup for supporting you’

kumbe unanichekea kinafiki na ulikua na mabomu yako umeyapanga kuyalipua ‘sawa mama angu ila mimi nimetoa ya moyoni mwangu kwako na naamini ujumbe utakufikia mana nimeshindwa kukaa na duku duku’sisi wote binadam na hatuna garantee ya kuishi’salute kwako kwa ulichofanya”.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment