Video: Kamati ya Uchaguzi CCM Hadharani

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kamati ya wajumbe 32 mahususi kwa ajili ya kempeni za Uchaguzi Mkuu 2015 chini ya Mwnyekiti Abdulrahman Kinana.

 Akizungumza na wanahabari katika Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam leo, Katibu wa Uenezi wa CCM amesema Kinana atasaidia jukumu hilo na makamu wenyeviti wawili; Rajabu Luhavi (Bara), Vuai Ali Vuai (Z’bar). Mbali na viongozi hao, kamati inaundwa na wajumbe wengine kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakiwemo makada Sophia Simba, Asha-Rose Migiro, Mwigulu Nchemba na Nape Nnauye. 

Wengine ni January Makamba, Stephen Wassira, Shamsi Vuai Nahodha, Lazaro Nyalandu, Bernard Membe, Ummy Mwalimu Pamoja na Makongoro Nyerere. 

Wanakamati wengine ni Maua Daftari, Mahmoud Thabiti Kombo, Christopher Ole Sendeka, Harrison Mwakyembe, Stephen Masele, Shaka Shaka na Pindi Chana. 

Wakati huohuo, Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi amesema Kamati Kuu ya CCM iwaidhinisha Jonathan Njau kuwa mgombea ubunge jimbo la Singida Mashariki pamoja Emmanuel John atakayepeperusha bendera ya CCM jimbo la Kiteto. 

Uchaguzi wa awali katika majimbo hayo ulilazimika kurudiwa baada ya chama hicho kutangaza kuwa kulikuwa taratibu zilivunjwa.

 Majimbo mengine ambayo CCM ililazimika kurudia kura za maoni ili kuwapata wagombea ubunge ni Rufiji, Busega, Makete, Ukonga na Kilolo.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment