JK: Wajumbe NEC Wana Kazi Kubwa







Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete jana alifungua Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho huku akikiri kuwa “wajumbe wana kazi kubwa”.
Kikao hicho kilikutana jana baada ya kupokea ajenda za Kamati Kuu iliyokutana juzi na jana, kujadili majina ya wagombea ubunge waliopitishwa katika kura za maoni na baadaye ingejadili ilani ya uchaguzi ya chama hicho, kama ilivyokasimishwa madaraka na Mkutano Mkuu wa Taifa.
Hata hivyo, Rais Kikwete alisema kazi ya wajumbe hao 362 kati ya 374 waliotarajiwa, ilipunguzwa na vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati Kuu ambavyo vilikutana na kuchambua majina na sifa za wagombea na kuwa iliyobaki haikuwa kubwa zaidi.
“Ndugu wajumbe habari za tangu tulipoachana katika mkutano wetu wa mwisho, leo tumekutana ili kufanya mchakato wetu wa mwisho wa kupata wagombea wa ngazi ya ubunge na ubunge wa viti maalumu pamoja na uwakilishi, kazi iliyoko mbele yetu ni kubwa,” alisema Kikwete.
Alisema kuwa kazi ya kuwapata wawakilishi katika vyombo vya dola inakuwa ni ngumu kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kugombea katika nafasi hizo.
“Idadi kubwa ya wagombea ndani ya CCM inaonyesha kuwa chama chetu kina mvuto, kwa hiyo tumekutana ili kufanya kazi hiyo na kazi iliyokwishafanyika ni kubwa kuliko kama ingekuja kwenu ikiwa mbichi kabisa, sasa tutatumia muda mfupi,” alisema na kushangiliwa.
Hata hivyo, alihoji idadi ya wajumbe wanaogombea ubunge ndani ya kikao hicho na idadi kubwa ya wajumbe walinyoosha mikono, jambo lililomfanya ashtuke na kuwatania kuwa, “tumebaki mimi na Kinana na Mzee Mangula ndiyo hatujagombea.”
Wakati wakianza, mjumbe mmoja, Michael Laizer alisimama na kumuomba mwenyekiti kuwa wakati wa upitishwaji wa majina, itapendeza wajumbe wanaogombea wasitoke nje wote badala yake watoke baada ya majimbo yao kutajwa.
“Mheshimiwa mwenyekiti, mimi napendekeza kuwa, wajumbe wasitoke nje tunapotaja mkoa husika, maana wakitoka tutakosa wa kutusaidia, badala yake naona wawe wanatoka wajumbe katika jimbo husika pekee ili wengine watusaidie katika mapendekezo,” alisema Laizer.
Kikao hicho kilifanyika wakati baadhi ya majimbo yakiwa hayajafanya uchaguzi baada ya matokeo yake kufutwa huku jimbo la Chilonwa mkoani Dodoma likuwa katika marudio ya kuhesabu kura baada ya mshindi wa pili, Deo Ndejembi kugomea matokeo.
Awali, Kamati maalumu ya CCM, Zanzibar ilikutana kuwajadili wagombea ubunge wa viti maalumu kutoka Zanzibar kwa kuwa hawakuwa wamewajadili na kikao hizo.
Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema ratiba ya mchako ilikuwa imebanana sana, lakini kila mgombea lazima atendewe haki.
Crdt: ,Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment