Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana ameugua ghafla wakati akiwa katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi chama hicho, Edward Lowassa baada ya kuchukua fomu za kugombea urais katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mbowe alishiriki katika maandamano yalioanzia makao makuu ya ofisi za CUF Buguruni wilayani Ilala jijini Dar es Salaam hadi NEC. Baada ya Mheshimiwa Lowassa kuchukua fomu, Mboewe alishiriki maandamano hayo kurejea makao makuu ya Chadema wilayani Kinondoni, lakini wakati akiwa njiani huku akiwa amechomoza kwenye gari la wazi, alikaa ghafla, na mwanasheria mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu na wenzake walimpatia huduma ya kwanza kwa kumfungua vifungo vya shati lake.
Baadaye alikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako alipatiwa matibabu. Akizungumzia hali hiyo, Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema kuwa Mbowe yuko salama na anaendelea vizuri.
“Ni uchovu, uchovu tu but he is out of ndanger )hayuko katika hali ya hatari),” alisema Lissu
Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema walimpokea Mbowe saa 11:00 jioni na alikuwa anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo. Hata hivyo hakutaka kuweka wazi ugonjwa uliokuwa unamsumbua.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment