Kiongozi wa Waasi wa Kundi la ADF Akamatwa Nchini Tanzania

Kiongozi mkuu wa kundi la waasi wa ADF wa nchini Uganda ametiwa mbaroni nchini Tanzania.
Vyombo vya habari vya nchini Uganda vimethibitisha kutiwa mbaroni kwa mtu anayeaminiwa kuwa ni Jamil Mukulu, mkuu wa kundi la waasi wa ADF ambalo linatuhumiwa kufanya mauaji ya watu 300 tangu lianzishe unyama wake katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Habari zinasema kuwa Mukulu ametiwa mbaroni kwa ushirikiano wa polisi wa Tanzania na wenzao wa Uganda.
Hata hivyo jeshi la Uganda limesema kuwa haliwezi kuthibitisha kuwa mtu aliyetiwa mbaroni ni Jamil Mukulu hadi atakapochukuliwa vipimo vya vinasaba, DNA.
Kwa muda mrefu polisi ya Uganda ilikuwa imetoa amri ya kutiwa mbaroni kiongozi huyo wa waasi wa ADF mwenye umri wa miaka 51 kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kigaidi na kuiomba jeshi la polisi la kimataifa kusaidia kumtafuta kiongozi huyo.
Kundi la ADF lilianzishwa mwaka 1995 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kupambana na siasa za Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment