Breaking News: Mamia Kumuaga John Nyerere Leo!! na Hii ndio Ratiba Kamili ya Mzishi

MAMIA ya wakazi wa Dar es Salaam leo wanatarajia kutoa heshima za mwisho kwa John Nyerere (58), ambaye ni mmoja wa watoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

John alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikokuwa amelazwa.Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto mwingine wa Mwalimu Nyerere, alisema Dar es Salaam jana kuwa mwili wa John utasafirishwa kesho kwenda Mwanza na kisha kupelekwa kijijini kwao Butiama Mkoa wa Mara kwa maziko.
Ratiba kamili hii hapa chini

“Misa ya kumuombea John itafanyikahapa Msasani nyumbani kwa Mwalimu na kufuatiwa na utoaji wa heshima za mwisho,” alisema Makongoro, ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

John alitumikia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na alishiriki Vita vya Kagera vya 1978 na 1979, vilivyolenga kumng’oa nduli Iddi Amin wa Uganda.

Watoto wengine wa Mwalimu ni Andrew, Magige, Madaraka, Anna na Rose.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment