Godbless Lema: Kuna Vichaa Wengi Mitaani


ARUSHA JOTO la Uchaguzi linazidi kupanda mjini hapa, baada ya vijana takribani 1,000 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika Jimbo la Arusha Mjini, kutangaza kutomsaidia Mbunge wao Godbless Lema wakati wa kampeni.

Vijana hao wakiongozwa na aliyekuwa dereva wa kwanza wa Lema ambaye pia alikuwa mratibu wa mawakala katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Rashidi Shuberti, wamekutana mjini hapa na kutangaza kupambana na mbunge huyo.

Wakati kundi hilo la vijana wakitangaza uamuzi wa kumwangusha Lema, Katibu wa Lema, Innocent Kisanyage aliliponda kundi hilo na kudai kuwa ni wahuni waliofukuzwa ndani ya Chadema siku nyingi.

Akizungumza na vijana hao jijini hapa jana Shuberti alidai alikuwa mstari wa mbele kwenye Kamati ya ushindi ya Lema mwaka 2010.

Alisema pamoja na kuongoza mapambano ya ushindi kwa kuwaongoza vijana wa Arusha Mjini sasa umefika wakati wameamua kupambana kuhakikisha Lema hashindi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktiba mwaka huu.

“Kwa bahati mbaya vijana wenzangu tuliaminishwa na kuanza kuhubiri Injili tusiyoijua ndani ya Chadema, kwani katika Injili hiyo wapo waliokufa, ndoa zao kuvunjika na wengine kupigwa risasi,” alisema Shuberti na kuongeza:

“Injili ile ya Chadema ilikuwa ni kupinga mfumo wa Chama cha Mapindizi (CCM), uliolazimisha haki na kanuni zivunjwe ili kuhalalisha mtu mmoja kuwa Meya wa Jiji la Arusha kinyume na kanuni na sheria,” alisema.

Alisema katika kupinga udhalimu huo alipewa jukumu la kuratibu maandamano ya kupinga matakwa ya CCM yaliyofanyika Januari 5, 2011 na kusababisha mauaji ya vijana watatu na majeruhi kadhaa. “Baadaye madiwani watano walifukuzwa katika chama kwa kumuunga mkono Meya Gaudence Lyimo.

Lakini miaka minne baadaye chama hicho hicho kikaa mezani kubariki mfumo kilioupinga na kusababisha vifo vya watu,”alisema Shuberti na kuongeza: “Nimetafari na vijana wenzangu tulivyopambana kumfikisha Lema alipo leo, tumehatarisha maisha yetu kwa asilimia 100.

Sasa kwa niaba ya wenzangu natangaza Lema hawezi kuwa Mbunge wa Arusha,”alisema . Shuberti alisema atahakikisha anashiriki kwa kiwango kile kile alichoshiriki kuhakikisha anamuangusha Dk. Batilda Burian aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CCM ili kuhakikisha Lema anashindwa uchaguzi.

MTANZANIA ilipomtafuta Lema kwa simu hakupokea na alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu na kuulizwa kama anamfahamu Shuberti alisema.

“Fedha ya CCM inaweza kutumika na vichaa wengi lakini haiwezi kuwasaidia CCM, Arusha hakuna CCM ila kuna bendera za CCM na muhimu CCM ifanye jitihada za kumpata mgombea ubunge, atakayeshindwa tena. “… kwani najua hawawezi kushindana na chama changu wala mimi hata kidogo kuna vichaa wengi mitaani,” alisema Lema
Credit: Mtanzania/Jf
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment