Breaking News:Yanayojiri Kituo cha Mabasi Ubungo

Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi leo asubuhi katika kituo cha mabasi ubungo jijini Dar es Salaam baada ya madereva ambao wanaendesha mgomo kuanza kuwarushia mawe baadhi ya viongozi waliofika kwa ajili ya mazungumzo na madereva hao akiwemo mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda na mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga.
Akiongea na EATV Afisa kutoka chama cha kutetea abiria, CHAKUA, bw, Gervas Lutaguzinda amesema kuwa madereva walianza kuwarushia mawe viongozi hao baada kudai kuwa ahadi wanazozitoa sio za msingi hivyo kutaka waziri mkuu afike eneo hilo.
Hata Hivyo Bw Lutaguzinda amesema kuwa hali kwa sasa imetulia na viongozi hao wanaendelea na mazungumzo na madereva hao ili kufikia muafaka wa tatizo hilo ambalo limefanya baadhi ya abiria kulala kwenye magari tangu jana.
Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe awasili kituo cha mabasi Ubungo na kupokelewa kwa shangwe na madereva
Crdt: EATV
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment