Vyama vya Siasa Nchini Vimeomba Ofisi ya Msajili Kutosuluhisha Migogoro ndani ya Vyama


Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Fransis Mutungi.Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Fransis Mutungi

VYAMA vya siasa nchini vimeiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama isihusike kutatua migogoro ya ndani ya vyama kwa kuwa jukumu hilo ni la ndani ya vyama husika vyenye miongozo ya kuitatua.

Badala yake, wameitaka ofisi hiyo ishughulike na utatuzi wa migogoro ya vyama inayohusisha chama kimoja na kingine, kwa sababu ndio wanayoamini kuwa inahitaji mtu wa pembeni wa kusimamia na kuongoza utatuzi.

Akizungumza katika mkutano wa mashaurino ya wadau wa vyama vya siasa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, uliodhaminiwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP), kwa lengo la kutafuta njia ya kufikia uchaguzi mkuu wa amani, Mwenyekiti wa chama cha Alliance for Tanzania Farmers (AFP), Said Sudi Said alisema.

Katika hatua nyingine Serikali imeombwa iiwezeshe ofisi hiyo kwa kuitengea bajeti ya kutosha isikwame kuendeleza jukumu lake la kuvipa vyama vya siasa uwezo wa kuendelea kuishi, kwa kuwa ndio mlezi anayetegemewa.

Kaimu Katibu Mkuu wa UDP, Isaack Cheyo alisema Ofisi ya Msajili ikiwezeshwa kifedha na kupatiwa watumishi wa kutosha itaweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha demokrasia ya vyama vya siasa nchini, hivyo kuwa na siasa za amani.

Kwa upande wake, mwakilishi wa CUF katika mkutano huo, Abdallah Mtolea alisema Ofisi ya Msajili haina budi kuongeza ushirikishwaji wa vyama vyote vya siasa katika masuala yanayogusa vyama ili kuvipa imani kuwa vyote vinathaminiwa.

CHANZO: Habari Leo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment